The Cross of Christ and an Antique Globe
Light of the Cross

HUDUMA YA JITANATION

YESU NI NJIA, NA KWELI,

NA UZIMA


"JOHN 14:6”


Man Carrying Haeavy Stone, Boulder Uphill.

'Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. '


MATHAYO 11:28 suv


Man Sitting and Reading the Bible

Safari yetu ya Imani

Jitanation tunaamini Yesu Kristo ni Bwana na Alifufuka katika wafu (Rum 10:9-12). Tunaamini Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, lenye uwezo wa kubadilisha maisha, kuponya mioyo, na kufanya upya nia. Tunaamini ya kwamba Yesu ndiye utimilifu wa Neno la Mungu lililofanyika mwili (Yohana 1:14) na Injili ya Yesu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye (Rum 1:16).



Yesu ni Njia, Na Kweli, Na Uzima

- Yohana 14:6

Lighted Light Bulb in Selective-focus Photography

maono yetu

01.

Kuona maisha ya watu kutoka matabaka na dini zote yakibadilishwa kwa nguvu ya Injili, na Ufalme wa Mungu ukisonga mbele katika kila nyanja ya jamii. Tunatazamia kuinua mabalozi wa Kristo katika familia, mahali pa kazi, biashara na kila nyanja za jamii...

02.

Kuona Maisha ya watu yakiponywa, kurejeshwa, kutiwa nguvu na jamii zikiathiriwa kwa nguvu ya Injili, Maombi, kuabudu...Nk.

03.

Kufikia watu wengi zaidi na kuhudumia watu wa Mungu kwa ukaribu zaidi kwa kurusha vipindi mubashara vya Injili ya Neno la Mungu, maombi na maombezi katika Mitandao ya kijamii na kuwa na mkusanyiko wa maombi ya pamoja, Kwa kadri Mungu atavyotuwezesha.

United in their business mission

misheni yetu

01.

Kuwezesha watu kutafuta uwepo wa Mungu na kujenga uhusiano wa karibu na Mungu. Tunaamini katika Nguvu ya Injili ya Yesu Kristo na Maombi katika kuleta badiliko kwenye maisha ya watu.

02.

Kuwezesha watu kukua kiroho kwa njia ya maombi, kuabudu, na kujifunza Neno la Mungu ili kuimarisha uhusiano wao na Mungu na kukua katika ufahamu wa Neno Lake.

03.

Kuwawezesha watu kuishi kwa imani katika kila eneo la maisha yao kupitia Injili ya Kristo.

Iwe wewe ni mpya katika imani au mzoefu kuna mahali pako Jitanation. Shiriki nasi kupitia mitandao ya jamii tunapotafuta uwepo wa Mungu na uweza wa Nguvu zake kwa Neno na Maombi katika safari yetu ya Imani.


- Jitanation

Orange background

sadaka

Unaweza kutoa sadaka yako ya hiari kwa ajili ya madhabahu hii, sadaka ya shukrani kwa yale ambayo Mungu amefanya kwenye maisha yako kupitia madhabahu hii au Nadhiri ambayo ulimuahidi Mungu kwa ajili ya Madhabahu hii.. Nk...


"Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. (2 Wakorintho 9:7-8 NEN‬‬)


Mungu akubariki

Gold Coins inside Glass Jar
Orange background

jitanation

"partners"

Kama umeguswa kuiwezesha Jitanation, Kufikia malengo yake, unaweza kufanya hivyo kwa kutoa sadaka yako ya Upendo kwa kadri Mungu anavyokuwezesha na Roho wa Mungu anavyokuongoza. Kila mchango, mdogo au mkubwa ni wa thamani sana na utatusaidia kufikia malengo ya Huduma Hii.


"Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa (Luka 6:38 SRUV).


Mungu akubariki

Gold Coins inside Glass Jar
Abstract Minimalist Dots Shapes

mawasiliano

Chat Message Icon

+255 747 191459

email icon

jitanation@gmail.com.

location glyph icon

P.O.Box, 90579, Dar-es-salaam.

Elegant Ornate Profile Picture Round Frame
Abstract Minimalist Dots Shapes
Abstract Minimalist Dots Shapes

NENO LA BARAKA

mungu

akubariki

Elegant Ornate Profile Picture Round Frame

' BWANA akubariki, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.' Hesabu 6:24-26 SRUV